Nyandu Toz afunguka sababu ya kuwa kimya

503
0
Share:
Narudi Narudi !!!! Hivyo ndivyo Msanii wa HipHop Nyandu Tozi alivyosema baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu sasa,huku akieleza sababu zilizomfanya kuwa kimya kwa kipindi takribani mwaka mmoja tangu alipotoa wimbo wa Kiboko ya Mabishoo aliomshirikisha msanii mwenzake wa Hiphop Cliff Mitindo.
Nyandu amesema sababu zilizomfanya kukaa kimya ni mazingira ya kimaisha tu, na hata hivyo alikataa kuweka wazi ni mazingira gani,akisema sio masuala ya kuweka hadharani
“Kuna Mazingira tu ya kimaisha yaliyonifanya niwe kimya,ila siwezi kusema hadharani ni mazingira gani,cha muhimu mashabiki wangu wajue kuwa narudi,” alisemaNyandu tozi
Msanii huyo ambaye ni miongoni mwa Wasanii wanaounda kikosi cha B.O.B,amesema hivi karibuni atarejea na tayari amesharikodi nyimbo za kutosha na kuongeza kuwa alikuwa akisubiri mfungo wa mwezi wa ramadhani kumalizika ili kuziachia Rasmi.
“Tayari nimeshafanya nyimbo nyingi tu,kuna nyimbo  ambayo nimeimba na David Genzi Young Dee, itatoka hivi karibuni,ila unajua tulikuwa katika mfungo wa mwezi wa ramadhani kwahiyo nilikuwa nasubiri umalizike,” aliongeza Nyandu
Ni wazi kuwa  kwa sasa soko la muziki wa bongofleva linaonekana kuwa na maslahi zaidi kuliko Hiphiop,wakati Nyandu Tozi akijipanga kurejea amejiandaaje 
“Unajua Hiphop ni feeling alafu ni mziki ambao unazungumzia ukweli na kama unavyojua ukweli unapingwa sana kwahiyo mimi narudi kuja kufanya muziki tu,ikitoea mambo ya maslahi tutajua baadae,” alizidi kufunguka Nyandu
Pia alizungumzia suala la kufanya Kolabo na msanii kutoka nje ya tanzania huku akisema kuwa katika nyimbo zake alizokamilisha hajafanya kolabo na msanii wa nje na hajafikiria bado
“Kufanya Kolabo na msanii wa nje bado na hata katika nyimbo zangu zilizokamilika sijamshirikisha msanii yoyote wa nje ya Tanzania labda kwa baadae,” alisema Nyandu
Nyandu Tozi anatajaria kurejea hivi karibuni na nyimbo za kutosha ambazo tayari ameshafanya na maproducer tofauti,lakini pia kuna ngoma ambayo amemshirikisha msanii mwenzake Young Dee.
Na Rahimu1993
Share:

Leave a reply