Nyoka asababaisha Emirates kuhairisha safari

2134
0
Share:

Shirika la Ndge la Emirates limeamua kuhairisha safari baada ya kugundua kuwa kuna nyoka katika ndege iliyokuwa inatakiwa kusaifirisha abiria kutokea Oman kwenda Dubai.

Safari hiyo yenye namba EK0863 ililikuwa ikianzia Muscat kwenda Dubai ilibidi isimamishwe muda mchache kabla ya abiria kuanza kuingia kwenye ndege baada ya wasimamizi wa ndege kukuta kuna nyoka ndani ya ndege jambo lililozua hali ya hofu hivyo ili kuepuka hatari inayoweza kujitokeza safari ikahairishwa.

Katika taarifa ambayo imetolewa na Emirates hawajafafanua ni aina gani ya nyoka ambaye amekutwa ndani ya ndege lakini alipatikana wakati wakikagua ndege kabla ya kuruhusu abiria waingie ndani ya ndege ili safari ianze.

Hii inakuwa sio mara ya kwanza kwa nyoka kukutwa ndani ya ndege kwani hata mwezi Novemba mwaka jana, ndege moja nchini Mexico ilikutwa na nyoka wakati ikiwa katika safari.

Share:

Leave a reply