Obama afurahi siku ya shukrani na wanawe kiaina

375
0
Share:

Rais wa Marekani, Barack Obama alinunua (ice cream) kwa ajili ya watoto wake wawili Malia na Sasha katika mgahawa wa Pleasant Popa kati kati ya mtaa mmoja wa maarufu wa biashara jijini Washington D.C

Wachambuzi wa mambo wanasema ilikuwa ni heshima kubwa kwa rais kuwanunulia (Ice Cream) watoto wake katika siku hii maarufu ya shukrani (Thanksgiving day)

Baada ya kuwatukimika wa Marekani kwa takribani miaka nane sasa Rais Obama anajiandaa kutoka madarakani kwenye ofisi za Oval “ Ni muhimu kwake kuwa na wanae katika siku ya shukrani,” amesema mmoja wa wakazi wa jiji hilo,”

Katika mtandao wa kijamii wa facebook alituma ujumbe na picha, Obama alionyesha jinsi watoto wake walivyokuwa kwa haraka katika ikulu ya White house, alituma picha wakati wanaingia kwa mara ya kwanza kwenye ikulu hiyo na ya sasa hivi.

“kwangu mimi nyumba hii ni sehemu iliyokuwa maisha yangu kwa maamuzi magumu na kupitia vipindi vigumu kama rais marekani, lakini ilikuwa faraja kuwa karibu na mke wangu Michele kama wazazi kuangalia watoto wetu wanavyokua katika maisha ya Amani, furaha kwa kweli ni familia bora,” amesema Obama

Share:

Leave a reply