Online TV zinafaida kubwa nchini-TCRA

190
0
Share:

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa, nchi imepiga hatua na kuwa ya mfano wa kuigwa baada ya ongezeko kubwa la ‘Online tv’ ambazo zimekuwa na faida kubwa ikiwemo kuongeza ajira pamoja na kuhabarisha umma kwa haraka zaidi kupitia sekta ya Mawasiliano.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Septemba 20,2017, jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa TCRA, Semu Mwakyanjala amesema kwa sasa kuna ongezeko la watumiaji wa Mtandao (Internet) wanaokadiriwa kufikia Milioni kumi na nane (Milioni 18) kwa sasa kutoka Milioni tano (5 Milioni) katika mwaka 2011.

“Kwa sasa watumiaji wameongezeka zaidi hadi kufikia Milioni 18, sasa humu kuna tv zingine za mtandaoni ‘Online TV’, kutuma miamala ya simu kwa kutumiana pesa na mambo mengine ikiwemo mitandao ya kijamii kama WhtsApp na mengine” alieleza Mwakyanjala.

Hata hivyo akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari kuhusiana na uwepo wa wingi wa tv za mtandaoni ‘Online tv’ kama ni tishio kwa usalama wa Mawasiliano?, Hata hivyo Kaimu Meneja huyo wa TCRA, Mwakyanjala alieleza kuwa: “Ujio wa Online tv sio tishio. Ni faida zaidi kwa sababu sasa hivi mwananchi hutakiwi kuwa nyumbani kwako ili uangalie tv, Popote upo barabarani unatakiwa kupata taarifa ‘up-to-date’  Yaani ni moja wapo ya mambo ambayo Serikali yetu imefanikiwa kuwaletea maendeleo wananchi wake kwani nchi zingine hakuna hivi vitu.

Athari hakuna, isipokuwa pale ambapo zitatumika vibaya ndio maana tunasema wananchi wasitumie kinyume hivi vitu. Kwa sasa sekta ya Mawasiliano imekuwa ni ya ajira na imekuwa chachu ya maendeleo ya ukuaji wa uchumi.” Ameeleza Mwakyanjala.

Mwakyanjala amebainisha hayo wakati wa kutoa taarifa kwa Umma kuhusu ufahamu wa matumizi sahihi na salama ya mitandao ya kompyuta na Intanet.

Ambapo aliweka wazi kuwa, kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao nchini (Tanzania Computer Emergency Response Team-TZ-CERT) kimepewa jukumu  la Kitaifa la kuratibu matukio ya usalama katika mitandao ya kompyuta na Intaneti kwa kushirikiana na vyombo vingine  vikiwemo vya Kikanda, kimataifa katika kusimamia matukio ya usalama mitandaoni.

“TZ-CERT ilianzishwa kwa sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010, kifungu namba 124. Kifungu  namba 5(1) cha kanuni za mawasiliano ya kielektroniki na Posta na kuzinduliwa rasmi 2015. Hivyo chombo hichi kina majukumu mengi ikiwemo kufuatilia shughuli za kiusalama mitandaoni hii ni pamoja na kutoa ushahuri wa kiusalama wa kukabiliana na masuala ya kiusalama. Kufanya uchambuzi na kutoa miongozo ya kitaalamu kwa umma na wadau na mambo mengine” alieleza Mwakyanjala.

Na Andrew Chale-MO BLOG

Video ya tukio hilo

Baadhi vichukua sauti vya tv za mtandaoni ‘Online Tv’ vikiwa tayari kwa tukio la mkutano

 Kaimu Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa TCRA, Semu Mwakyanjala akionesha moja ya taarifa zilizomo kwenye kitabu cha TCRA kinachoelezea usalama wa mitandaoni. kulia kwake ni Afisa wa Idara habari MAELEZO.

 Kaimu Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa TCRA, Semu Mwakyanjala akizungumza katika tukio hilo juu ya ufahamu wa masuala ya matumizi sahihi na usalama wa mitandao ya kompyuta nan Intaneti. (Picha na MO BLOG).

Share:

Leave a reply