Papa Francis akataa kuongeza walinzi

543
0
Share:

Licha ya sehemu nyingi duniai kuonekana kutokuwa na uhakika wa usalama, hali hiyo inaonekana kutokumpa hofu Papa Francis kwani ameweka wazi kabisa kwamba hana hofu na hali hiyo pindi atakapokuwa akifanya ziara katika mataifa mbalimbali.

Papa Francis amesema anatambua kuwepo hali ya hatari katika maeneo mbalimbali lakini yeye hana hofu ila ana wasiwasi juu ya watu ambao anatembea nao na watu ambao anakutana nao katika ziara zake.

“Nafahamu juu ya hatari ambayo inaweza kujitokeza, Labda mimi sipo sawa lakini lazima niseme sina woga wowote kuhusu mimi, nina wasiwasi kuhusu usalama wa wale ambao wanasafiri na mimi,

“Zaidi ya yote ni kwa wale watu ambao nakutana nao katika nchi mbalimbali. Kuna ishara ya hatari kwa mtu mwenye matatizo ya akili lakini siku zote Bwana yupo,” alisema Papa Francis.

Tangu alipochaguliwa mwaka 2013, Papa Francis ameshafanya ziara katika mataifa zaidi ya 25.

Share:

Leave a reply