PICHA: Nyumba ya gharama zaidi Marekani, inauzwa Bilioni 560 za Kitanzania

2316
0
Share:

Msemo wa maisha ni nyumba na wengine wakisema hakuna baba mwenye gari kuna baba mwenye nyumba unaweza kuwa na maana kwa namna moja au nyingine ya kuonyesha nyumba kuwa na thamani kubwa tofauti na wengi wanavyofikiria.

Nchini Marekani kunajulikana kuwepo na watu wengi na wenye uwezo wa kifedha jambo ambalo linafanya kuwepo na nyumba za gharama kubwa ambazo ujenzi wake pia unakuwa wa thamani kubwa na mara nyingi hununuliwa na watu matajiri wanaopenda kuishi katika nyumba za kifahari.

Kwa mwaka 2017 nyumba ambayo inatajwa kuuzwa kwa pesa nyingi zaidi inatajwa kufikia Dola milioni 250 ambazo kwa pesa ya Tanzania inafika Bilioni 560.

Nyumba hiyo ina vyumba 12 vya kulala, mabafu 21, sehemu ya kunywa vinywaji tano, majiko matatu, sehemu ya kutizama filamu, bwawa la kuogelea, chopa na mengine mengi ambapo ujenzi wake umefanyika kwa miaka minne.

 

 

Share:

Leave a reply