PICHA: Rais Magufuli aongoza mamia ya Watanzania kuaga mwili wa Samuel Sitta

Mwili wa aliyekuwa spika wa bunge la Tanzania, Samuel Sitta umeagwa katika viwanja vya Karimjee na mamia ya watanzania wakiongozwa na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais mama Samia Suluhu.
Wengine ni Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Gharib Bilal, Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye, Spika wa bunge aliyepita, Anna Makinda, Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka na viongozi wengine wa ndani na mabalozi wa nchi mbalimbali.
Mwili wa mzee Sitta ulifika majira ya saa mbili asubuhi kwa msafara wa heshima ya kiserikali na kuagwa na watu mbalimbali ambao walifika viwanja vya Karimjee.
Sitta alifariki Jumatatu ya Novemba, 7 akiwa katika matibabu nchini Ujerumani ambapo alikuwa akisumbuliwa na saratani ya tezi dume, mwili wake uliwasili nchini jana Alhamisi na baada ya kuagwa Dar, mwili wake utapelekwa Dodoma kwa ajili ya wabunge kutoa salamu za mwisho kisha kupelekwa Urambo, Tabora.
PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE