PICHA: Rais wa FIFA awasili nchini kwa mara ya kwanza

447
0
Share:

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino amewasili nchini kwa ajili ya mkutano wa FIFA unaofanyika hapa nchini katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.

Infantino amewasili nchini alfajiri ya Alhamisi ya Februari 22 akiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad na kupokelewa na Waziri wa Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na viongozi mbalimbali wa soka akiwepo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Wallace Karia.

Share:

Leave a reply