PICHA: Rais wa Shirika la Engender Health alivyokutana na Waziri wa Afya wa Zanzibar

140
0
Share:

Visiwa vya Zanzibar vimepata ugeni wa Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Engender Health, Ulla Muller lenye makazi yake nchini Marekani na akiwa visiwani humo amepata nafasi ya kukutana na Waziri wa Afya Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo.

MO Blog imekuandalia picha kuona jinsi Waziri Kombo alivyokutana na Ulla Muller.
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akiahidi mashirikiano ya karibu na Shirika la Engender Health wakati wa mazungumzo yake na Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Ulla Muller Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Rais wa Shirika la Engender Health la Marekani Ulla Muller ambae pia ni Mtendaji Mkuu (CEO) wa Shirika hilo akizungumza na Waziri wa Afya  Mahmoud Thabit Kombo alipomtembelea Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar, (kulia) ni Mkurugenzi Ufundi ambae ni Naibu mwakilishi wa Shirika hilo Tanzania Feddy Mwanga.

Share:

Leave a reply