PICHA: Timu ya Gofu ya NMB yashiriki mashindano ya Tanzania Open Kili Golf

458
0
Share:

Timu ya mchezo wa Gofu ya Benki ya NMB inashiriki michuano ya Tanzania Open Kili Golf ambayo yanafanyika mkoani Arusha.

Akizungumza kuhusu machuano hiyo, kapteni wa timu hiyo, George Kivaria alisema wachezaji wa NMB ambao wameshiriki mashindano hayo ni watano lakini pia benki ya NMB imetoa udhamini kwa wachezaji 12 wa timu ya Jeshi Mgulani.

Alisema lengo la kushiriki pamoja na kuwa sehemu ya udhamini wa michuano hiyo ni kuwa karibu na jamii wanayoihudumia na kuahidi kuendelea kudhamini michezo mbalimbali nchini.

Tanzania Open Kili Golf imeshirikisha zaidi ya wachezaji 240 kutoka hapa nchini na mataifa mbalimbali kama Zambia, Malawi, Kenya, Uganda na Afrika Kusini.

 

Share:

Leave a reply