Picha za utupu zawatesa wabunge Kenya

254
0
Share:

Wabunge wa Kenya wamedai kuvamiwa na wahalifu wa mtandaoni, ambao huwatumia picha za utupu katika simu zao kwa lengo la kuwashawishi kuwapa fedha.

Wabunge hao walitoa madai hayo jana Jumanne ambapo walielezea jinsi wanavyosumbuliwa na wahalifu hao.

Kiongozi wa walio wengi Bungeni, Aden Duale na Mbunge wa Kiminini, Chris Wamalwa walilielezea Bunge la Kenya namna ambavyo mwanamke mmoja nchini humo amekuwa akiwatumia picha hizo kwenye simu zao , kitendo kinachowapa hofu kutumia simu hadharani.   

Wamalwa amedai kuwa, suala hilo limevunja familia nyingi na kwamba ni lazima lishughulikiwe.

Share:

Leave a reply