Polisi India wawashikilia wanaume wanne kwa ubakaji wa mtalii wa Marekani

370
0
Share:

Polisi wa India wamewakamata wanaume wanne nchini humo  pamoja na kijana mpiga kengele wa hoteli ya nyota tano katika ya mji wa India siku ya Jumatatu kwa tuhuma za kumbaka mtalii kutoka Marekani mwezi wa Aprili.

Polisi wanasema kwamba kabla ya kumbaka mtalii huyo wa Marekani walimjeruhi vibaya sehemu za usoni na wachunguzi wa mambo wanasema tukio hilo linazidi kuichafua nchini ya India katika duru za kimataifa hasa kwa usalama wa wanawake.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni mtalii kutoka nchini Marekani ambaye alipeleka malalamiko yake rasmi mwezi wa Oktoba, na aliweza kurudi ili kutoa ushahidi mbele ya mahakama na kuwatambua watuhumiwa, gazeti la Times la India liliripoti.

Baada ya kupata ushahidi kutoka katika taasisi isiyo kuwa ya kiserikali kutoka nchini mwake kwa niaba ya muathirika, Polisi nchini huo waliwatia mbaroni vijana wao kwa mashtaka ya ubakaji.

“Bado tunaendelea kuwahoji wanaume hawa wanne na bado tuna msaka mtuhumiwa wa tano ambaye ametoroka,” alisema Mkuu wa Polisi katika mji wa New Delhi,”

Kwa mujibu wa ofisa wa Polisi, kwa maelezo ya muathirika wa tukio ni kwamba watu watano wakiwa wamelewa pombe walimbaka na kumpiga sehemu zake za mwili ndani ya chumba chake cha hoteli aliyofikia.

Share:

Leave a reply