Polisi Uganda wakataa kutekeleza agizo la Rais Museveni

1346
0
Share:

Yawezekana lisiwe jambo la kawaida lakini haina jinsi kwa polisi wa Uganda kuamua kufanya maamuzi magumu ya kukataa kufanyia kazi agizo lililotolewa na Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni la kuacha kuzuia magari mengine kutumia barabara muda ambao anakuwa anapita katika eneo hilo.

Agizo hilo ambalo lilitolewa na Rais Museveni mwezi Februari mwaka huu aliagiza polisi kuruhusu watu wengine kutumia barabara hata kama na yeye atakuwa anatumia barabara za maeneo mbalimbali nchini humo.

Jambo hilo linaonekana kuwa tofauti kwa polisi kwani tangu agizo lilipotolewa hakuna utekelezaji uliofanyika, Mkuu wa jeshi la polisi la Uganda, Jenerali Kale Kayihura amesema sababu ya agizo hilo kutokufanyiwa kazi ni kuhofia usalama wa Rais.

“Kwa hakika hatukutakiwa kumfungulia njia apitapo lakini imetubidi kufanya tofauti na hivyo kwa ajili ya usalama wake na hiyo ndiyo sababu ya yeye kutuonya sisi kwanini hatutekelezi agizo lake,” alisema Jenerali Kayihura.

Share:

Leave a reply