Polisi waanza uchunguzi wa kifo cha kiongozi wa Chadema

104
0
Share:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, RPC Jumanne Mlilo amesema Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wa kifo cha Katibu wa Chadema Kata ya Hananasifu, Daniel John ambaye mwili wake ulikutwa kwenye ufukwe wa Coco Beach baada ya kutoweka.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, RPC Mlilo amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo jana Februari 13, 2018 kutoka kwa msamaria mwema aliyetoa taarifa katika kituo cha Osterbay.

“Taarifa tulizozipata ndizo tunazifanyia kazi tujue aliyekufa ni nani na chanzo cha kifo chake ni nini,” amesema.

Amesema Jeshi la Polisi lilituma askari kwenda eneo la tukio na kukuta mwili wa mtu mwenye jinsi ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35 ukiwa na majeraha kichwani, usoni, mkononi na miguuni yanayoashiria kuwa amepigwa na kitu chenye ncha kali.

Katika hatua nyingine, RPC Mlilo amesema itakapolazimika wataichunguza kauli ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kujua kauli yake hiyo ilikuwa ina maanisha nini au ilisukumwa na hisia zake.

“Kauli yake pia tunaichunguza ili tujue inatumia misingi ipi kwa kile anachosema, hatuwezi kumuacha mtu azungumze kutokana na hisia za mtu, hatuwezi tukatoka kwenye misingi ya sheroia kwa kusukumwa na hisia za mtu,” amesema Mlilo.

Share:

Leave a reply