Polisi waanza utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli

669
0
Share:

Jeshi la Polisi Nchini limeanza kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kuwachukulia hatua viongozi waliotajwa kwenye ripoti ya Uchimbaji Madini ya Tanzanite na Almasi , aliyokabidhiwa jana Ikulu Jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 8, 2017 jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,, IGP Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vyengine vya ulinzi limeunda kikosi kazi cha kushughulikia ripoti hiyo. 

“Baadhi ya watuhumiwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa kwa lengo la kukusanya ushahidi na hatimaye wafikishwe mahakamani,” amesema.

Katika hatua nyingine, IGP Sirro amesema Jeshi la Polisi linaendelea kufanya upelelezi wa tukio la mlipuko uliotokea katika ofisi za Mawakili wa IMMA lililotokea Agosti 20 mwaka huu, na kwamba upelelezi ukikamilika wahusika watafikishwa mahakamani.

Pia amesema Jeshi la Polisi limewakamata wahusika wa tukio la utekaji wa watoto lililotokea mkoani Arusha Septemba 4, 2017 na Geita Septemba 1 mwaka huu. Amesema upelelezi unaendelea ili kuwabaini waliohusika katika matukio hayo.

Na Regina Mkonde 

Share:

Leave a reply