Polisi watatu wauawa kwa kupigwa risasi Misri

226
0
Share:

Polisi watatu wameuawa na wengine watano kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kueleza kuwa wahusika wa tukio hilo waliwapiga risasi askari hao wakiwa kwenye pikipiki katika eneo la barabara kuu ya Nasr City.

Wizara imeeleza kuwa tukio hilo limetokea jumatatu usiku na mpaka sasa hakuna kikundi chochote cha kigaidi ambacho kimedai kuhusika na mauaji hayo.

Kwa sasa nchi ya Misri ipo katika hali ya hatari baada ya mwezi uliopita Rais Abdul Fattah al-Sisi kutangaza hali hiyo kufuatia watu 45 kuuliwa katika makanisa mawili yaliyopo nchini humo.

Share:

Leave a reply