Polisi yaua majambazi watatu, Waziri Kitwanga aelezea mkakati wa serikali (Audio)

184
0
Share:

Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua majambazi watatu baada ya kurushiana risasi katika tukio la ujambazi lililofanyika katika benki ya Access tawi la Mbagala Rangi Tatu.

Simon Sirro

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Akielezea tukio hilo, Kamanda wa Polisi, Simon Sirro alisema majambazi wanaokadiriwa kufikia 12 walivamia benki ya Access na kumwua askari mwenye namba H7739 PC Halid na mwenzake PC Shaban kasha kuingia ndani na kuwajeruhi watumishi wa benki hiyo ambao ni Afisa Mikopo, Salum Juma na Francis Amani kisha kupora kiasi cha pesa kinachokadiliwa kufikia Milioni 20 na 30.

Baada ya kufanya tukio hilo majambazi hao walikimbia na ndipo walipokutana na vikosi vya polisi ndipo walipoanza kurushiana risasi ndipo Polisi walipofanikiwa kuwaua majambazi watatu na wengine kukimbia katika msitu wa Kongowe.

“Tulifanikiwa kuwaua majambazi watatu na kufanikiwa kukamata pikipiki sita, SMG tatu za kwetu mbili ambazo waliwanyanganya askari wetu na upelelezi wa nguvu sana unafanyika ili kuweza kuwakamata na tunataka kuhakikisha tunakamata mtandao wote unaovamia katika mabenki unakamatwa,” alisema Kamanda Sirro.

Katika matukio mengine mawili tofauti Polisi wamefanikiwa kukamata majambazi watatu wakiwa na bastola aina ya browing na askari bandia wanne wakiwa na sare za jeshi hilo, redio upepo (radio call) na pingu.

Aidha Kamanda Sirro amewataka wananchi kuwafichua waharifu wote ambao wamekuwa wakijificha katika jamii na Jeshi la Polisi litawachukulia hatua watu hao ili kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Aidha Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Charles Kitwanga alisema serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha inawamaliza majambazi ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikigharimu maisha ya wanadamu.

Charles Kitwanga

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Charles Kitwanga akitoa taarifa kuhusu mpango wa serikali kufuatia tukio la majambazi kuvamia benki ya Access.

“Niwaombe wananchi waungane na sisi tumeamua na sisi tunataka kufanya hivyo kwa njia njema ili kuhakikisha tunamaliza mtandao wote na majambazi, natoa onyo kwa hawa watu wasidhani kuwa tumelala,” alisema Waziri Kitwanga.

Pia Kitwanga amesema kuwa atazungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi ili kushirikiana kuona ni jinsi gani wanaweza kushirikiana kufanya doria katika pori la Pwani sehemu ambayo inaonekana majambazi wengi kukimbilia huko.

Kamanda wa Polisi, Simon Sirro

Kamanda wa Polisi, Simon Sirro

Kamanda wa Polisi, Simon Sirro Kamanda wa Polisi, Simon Sirro Kamanda wa Polisi, Simon Sirro Kamanda wa Polisi, Simon Sirro

Share:

Leave a reply