Producer wa Alicia Keys kufanya kazi na msanii wa Kenya, Wyre

235
0
Share:

Katika kukuza tasnia ya muziki nchini Kenya, Mwanamuziki  Kevin Wyre ‘ Wyre’  ameamua kumshirikisha muongozaji kutoka nchini Marekani kama sehemu ya kujenga mahusiano mazuri na waongozaji wa muziki wa nchi za nje.

Muongozaji huyo anayejulikana kwa jina la Carlo Montagnese, maarufu kama Illangelo, aliyewahi kushinda tuzo za Grammy kama muongozaji bora, mwandishi bora na mtaalamu wa kuchanganya muziki.

Wyre amesema kwamba muziki wake unahitaji kitu cha tofauti kama sehemu ya kuuboresha na kuweza kutengeneza uhusiano mzuri na waongozaji wa nje ya nchi, huku akiwataka mashabiki wake kukaa tayari kupokea kibao chake kipya kilicho andaliwa na mwongozaji huyo.

illangelo

Carlo Montagnese.

“Muziki wangu nitaufanya uwe watofauti kidogo, lakini pia nafanya na muongozajo Illangelo sio kwamba waongozaji wa kenya hawawezi lakini nikutengeneza mahusiano mazuri na waongozaji wanje ya nchi.” Amesema Wyre.

Aidha ameongezea na kusema kwamba nimatumani yake kibao chake hicho kipya kitakosha nyoyo za mashabiki wake kwani ana imani na muongozaji Illangelo kutokana na kazi zake nyingi alizo zifanya na mwanadada Alicia Keys ikiwemo wimbo wa “In common”, “28 thousands days” na “Hallelujah”.

Share:

Leave a reply