Prof. Mbarawa amemteua Mhandisi Deusdedit Kakoko kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA

361
0
Share:

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame M. Mbarawa, leo tarehe 25 Juni, 2016 amemteua Mhandisi Deusdedit Conatus Vitalis Kakoko kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Mhandisi Kakoko amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Ephraim Mgawe ambae uteuzi wake ulitenguliwa.

Mhandisi Kakoko ni Meneja wa miradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Ramsey V. Kanyanga

KAIMU KATIBU WA WAZIRI

25/06/2016

Share:

Leave a reply