Qatar yaongezewa muda kufanyia kazi masharti iliyopewa na nchi nne za kiarabu

616
0
Share:

Baada ya kumalizika kwa siku 10 ambazo ilipewa Qatar kufanyia kazi masharti 13 ambayo iliwekewa na nchi zingine nne za Kiarabu zimemalizika Jumapili ya Juni, 2, maagizo mengine yametolewa.

Nchi nne za kiarabu ambazo ni Saudi Arabia, Misri, Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain zimeiongezea Qatar saa 48 yaani siku mbili kufanyia kazi masharti ili iondolewe vikwazo iliyowekewa.

Vikwazo hivyo ni pamoja na kuzuia safari zote za anga, barabara na hata bahari za kwenda na kutoka Qatar.

Jumamosi ya Juni, 1 Waziri wa mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman alisema kuwa hawawezi kutekeleza masharti hayo lakini wapo tayari kufanya mazungumzo ambayo yatakuwa ya haki kwa pande zote mbili.

Share:

Leave a reply