Qatar yatengwa na nchi za kiarabu kwa tuhuma za kuunga mkono ugaidi

562
0
Share:

Mataifa sita ya kiarabu, ikiwemo Saudi Arabia, Misri, Bahrain, Umoja wa Milki za Kiarabu na Yemen, yamevunja uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar zikiishutumu nchi hiyo kuunga mkono ugaidi.

Mataifa hayo yameishutumu Qatar kwa kuunga mkono makundi ya kigaidi likiwemo kundi la Islamic State (IS). 

Aidha, Shirika moja nchini Saudi Arabia limesema kuwa taifa hilo limefunga mipaka yake na kusitisha usafiri wa ardhini, baharini na angani ikiwa ni hatua ya kulinda usalama wake kutokana na hatari za ugaidi na itikadi kali.

Saudi Arabia ilikuwa nchi ya kwanza kutangaza kuvunja mahusiano yake na Qatar  ikifuatiwa na Bahrain, Muungano wa Miliki za Kiarabu, Misri na Yemen.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply