Raia wa Syria kuruhusiwa kwenda eneo la kupata misaada ya kibinadamu

165
0
Share:

Jeshi la Urusi limesema waasi nchini Syria wameahidi kuruhusu raia waondoke eneo la Ghouta Mashariki jirani na mji mkuu wa Damascus ili waende eneo ambalo watapata misaada ya kibinadamu katika eneo hilo.

Mapema Urusi ilianzisha usitishaji mapigano katika eneo hilo lililoathiriwa zaidi na mashambulizi ya mabomu, lakini jeshi la Syria na waasi nchini humo wamekuwa wakiwazuia wakazi wa eneo hilo kuondoka.

Haya yanajiri wakati vikosi vya serikali ya Syria vikifanya mashambulizi mapya Ghouta Mashariki na kuwaua raia 14 usiku wa kuamkia leo.

Mashambulizi haya ya hivi karibuni yanafanya raia waliouawa hadi sasa kufikia 709 tangu vikosi vya serikali ya Syria na washirika wake Urusi walipozidisha mashambulizi yao dhidi ya Ghouta Mashariki kuanzia mwezi Februari mwaka huu.

Share:

Leave a reply