Rais Dkt. Magufuli ashirirki Dhifa ya Kitaifa na mgeni wake Rais Kagame

283
0
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuandalia Dhifa ya Kitaifa Rais wa Rwanda, Mh. Paul Kagame na mkewe Mama Jeannette Kagame Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Kagame alikuwa nchini kwa ziara ya Kikazi. Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali yaliyojiri katika Dhifa hiyo ya Kitaifa.

Magufuli and Kagame's

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akigonganisha bilauri na Mke wa Rais wa Rwanda, Mama Jeannette Kagame katika kusherehekea Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame (katikati) Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Kagame alikuwa nchini kwa ziara ya Kikazi.

Paul Kagame na Samia Suluhu Hassan

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia) akigonganisha bilauri na Rais wa Rwanda Paul Kagame, katika kusherehekea Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mgeni wake Rais Kagame. Dhifa hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.

Magufuli na Kagame

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mh. Kagame

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa amesima kutoa heshima wakati wa Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais Kagame (kulia kwake). Kulia ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. Wa pili kulia ni Mke wa Tanzania Mama Janet Magufuli na kushoto ni Mke wa Rais wa Rwanda, Jeannette Kagame.
Ali Hassan Mwinyi na Salim Ahmed Salim
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto) akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim (wa pili kushoto), Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman (wa tatu kulia) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo (kulia).
Joseph Sinde Warioba na Tulia Ackson
Waziri Mkuu Mstaafu Jiji Mstaafu Joseph Sinde Warioba akimsikiliza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Dkt. Tulia Ackson wakiwa kwenye Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa mgeni wake Rais Kagame. Dhifa hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mohamed Othman Chande na Ramadhan Madabida
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida wakiwa kwenye Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame aliyetembelea Tanzania kwa ziara ya Kikazi.
John Kijazi na Anna Makinda
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (kushoto) akiwa na Spika Mstaafu Anne Makinda (kulia), wakimsilikiza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage.
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeir
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeir (kushoto) akizungumza na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhad Musa Salum (katikati).
John Pombe Magufuli
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwenye Dhifa ya Kitaifa aliyoiandaa kwa ajili ya mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku. Katikati nini Mke Kagame, Mama Jeannette Kagame.
Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwenye Dhifa ya Kitaifa aliyoiandaa kwa ajili ya mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame (wa tatu kushoto) Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku. Kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anayemfuatia ni Mke wa Rais wa Tanzania mama Janet Magufuli na wa pili kulia ni Mke Kagame, mama Jeannette Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza kwenye Dhifa Dhifa ya Kitaifa aliyoiandaliwa na mwenyeji wake Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto). Kulia ni Mke wa Rais wa Tanzania, mama Janet Magufuli na wa pili kushoto ni Mke Kagame, mama Jeannette Kagame.
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria Dhifa ya Kitaifa
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame, Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku, wakimsikiliza Rais Kagame (hayupo pichani).
Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame akimsalimia Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Katikati ni Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.
Salim Ahmed Salim
   Rais wa Rwanda Paul Kagame akimsalimia Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (katikati). Kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Magufuli na Mwinyi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Balozi wa China Nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (wa pili kushoto) akimtambulisha Balozi wa China Nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing kwa mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Dkt. Tulia Ackson na Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Dkt. Tulia Ackson.Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Jiji Mstaafu Joseph Sinde Warioba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akimtambulisha Spika Mstaafu Anne Makinda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akimtambulisha Spika Mstaafu Anne Makinda kwa mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Magufuli na Kagame burudani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akiwana mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame, wakiangalia burudani ya kikundi cha Matarumbeta.
Magufuli akiagana na Kagame
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akimsindikiza Mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame (wa pili kulia) baada ya kumalizika kwa Dhifa ya Kitaifa.
Mwinyi na Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi wakati wakiondoka kwenye ukumbi wa Ikulu.
Magufuli na Salim Ahmed Salim

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (katikati) wakati wakiondoka kwenye ukumbi wa Ikulu.Wa pili kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Jiji Mstaafu Joseph Sinde Warioba na kulia ni Mke wa Rais Mama Janet Magufuli. (Picha na Hussein Makame-MAELEZO).

Share:

Leave a reply