Rais Dkt. Magufuli atembelea wagonjwa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mapema leo Novemba 10.2016 ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kujulia hali wagonjwa mbalimbali akiwemo mke wake, Mama Janeth Magufuli, ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali mke wake, Mama Janeth Magufuli, ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri wa Zamani Balozi Ramadhani Mapuri ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuri baadhi ya madaktari na wauguzi kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wananchi alipokuwa akitoka Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwafariji baadhi ya wagonjwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea kuona wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu hapo leo Novemba 10, 2016.Picha na IKULU