Rais Donald Trump atamani kuwa rafiki wa Kim Jong-un

600
0
Share:

Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi kuwa moja ya jambo ambalo anatamani ni kuwa rafiki wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Kauli hiyo ya Trump imekuja katika kipindi ambacho watu wengi wanaamini kuwa viongozi hao wawili wa mataifa yenye nguvu ya kiuchumi na silaha hawana uhusiano mzuri kutokana na mara kadhaa kurushiana maneno.

Trump ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa anatamani kuwa rafiki wa Kim Jong-un na anaamini ipo siku jambo hilo litafanikiwa.

“Kwanini Kim Jong-un ananitusi kwa kuniita “mzee”, wakati sijawahi kumwita “mfupi na mnene?”, Ooh vizuri, najatahidi sana kuwa rafiki yake na labda siku moja itakuwa hivyo!” aliandika Trump.

Share:

Leave a reply