Rais Magufuli akutana na Balozi wa Denmark na Rais Mkapa Ikulu Dar

365
0
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Januari, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Denmark hapa nchini Mhe. Einar Hebogard, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.

Mhe. Martin Bille Herman amesema katika mazungumzo hayo wamejadili kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Denmark na pia wamekubaliana kuuimarisha zaidi hususani katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Mkapa amesema lengo la kukutana na Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kumpa taarifa juu ya kazi anayoendelea kuifanya ya kuwa mwezeshaji wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzi na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.

Share:

Leave a reply