Rais Magufuli amteua Prof. Yunus D. Mgaya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR

456
0
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 17 Desemba, 2016 amemteua Prof. Yunus D. Mgaya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
Uteuzi wa Prof. Yunus D. Mgaya unaanza mara moja.

Prof. Yunus D. Mgaya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Mwele Malecela ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam mapema leo 17 Desemba, 2016

prof-_yunus_mgaya

Prof. Yunus D. Mgaya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ambaye ameteuliwa mapema leo

Share:

Leave a reply