Rais Magufuli amuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango leo

452
0
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 15 Desemba, 2016 amemuapisha Dkt. Khatib Malimi Kazungu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Dkt. Khatib Malimi Kazungu anachukua nafasi iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bw. Doto James kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Khatib Malimi Kazungu alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara iliyopo katika Mkoa wa Mtwara.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Bw. Jaffar Haniu, Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam

 

Share:

Leave a reply