Rais Magufuli apongezwa kwa kuwachukulia hatua watumishi walevi

259
0
Share:

Askofu wa kanisa la Pentekoste Tanzania (FPCT) Manispaa ya Singida, Dk. Paulo Samwel, amempongeza rais Dk.John Pombe Magufuli kwa kitendo chake cha kutumbua majipu hadi ya ulevi unaofanywa na baadhi ya watumishi wa umma wakati wa kazi.

Amedai hatua hiyo ambayo hakumbuki kama imewahi kufanywa na kiongozi yoyote wa toka nchi ipate uhuru, amewaunga mkono baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini ambao muda mwingi wamekuwa wakikemea matumizi ya pombe.

Dk. Paulo ametoa pongezi hizo juzi mbele ya waumini wa kanisa la kati la Pentekoste mjini Singida, waliohudhuria ibada ya kawaida.

Akisisitiza, alisema kwa ujumla pombe ina madhara mengi ikiwemo kurudisha nyuma maendeleo ya mhusika, kudhorotesha afya, kusababisha vifo, kumsababishia mtu asiwe na maamuzi sahihi na ambaye zaidi, kunywa pombe ni dhambi mbele ya Mwenyezi Mungu.

“Baada ya Rais wetu Magufuli kuonyesha wazi tena kwa vitendo kwamba serikali yake haitakuwa na nafasi na mtumishi wa umma anayelewa kazini, kitendo hicho huenda baadhi ya watumishi wa umma wakaichukia pombe na kuacha kabisa kuinywa. Kutokana na matunda hayo, ndio maana nasema rais wetu ametuunga mkono sisi viongozi wa dini katika kukemea matumizi ya pombe,” alisisitiza zaidi.

Katika hatua nyingine, Dk. Paulo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha Watanzania wote kupitia dini zao, kuendelea kuliombea taifa liendelee kudumisha amani na utulivu, ili wananchi wake waendelee kuabudu na kujiletea maendeleo kwa uhuru mpana.

“Tuendelee pia kuombea kundi hili kubwa la vijana ili kwenye midomo yao kusiwepo kiroba. Vijana kama tunavyojua ni nguvu kazi ya familia na taifa pia, wasipojiingiza katika kunywa viroba au pombe za aina mbalimbali, manispaa yetu ya Singida na nchi kwa ujumla, itapiga hatua kubwa kimaendeleo ya kijamii na nyumba zetu za ibada zitapata sadaka zitakazokidhi mahitaji ya ustawi wa nyumba hizo,” alisema askofu huyo.

Muumini wa kanisa hilo, Mama Lessi Jaredi, pamoja na kumpongeza askofu Dk. Paulo Samwel kwa kutoa wosia mzuri wa kimwili, alisema pombe ni adui mkubwa wa maendeleo ya kijamii na inachangia wahusika kujiingiza kwenye vitendo vya uzinzi ambavyo vinachangia wahusika kupata maambukizi ya magonjwa ikiwemo ugonjwa hatari wa UKIMWI.

“Pombe inasababisha kaya kuwa maskini na wakati mwingine inachangia ndoa nyingi kuvunjika. Watanzania sote bila kujali imani zetu za dini au itikadi zetu za kisiasa, tumuunge mkono rais wetu Magufuli kupiga vita mambo mabaya ikiwemo unywaji wa pombe. Kwa njia hiyo, nchi yetu itaendelea kuwa kisima cha amani,” alisema.

Muumini mwingine, Peter Paulo Samwel, ametoa wito kuandaliwa kwa semina mbalimbali zitakazotumika kutoa elimu juu ya madhara yatokanayo na unywaji wa pombe. Vijana wakiwa na ufahamu wa madhara ya pombe, wataacha kunywa pombe ya aina yoyote.

Kwa upande wake Metusela Kisuda, ameiomba serikali ya awamu ya tano ikaze kamba isiruhusu kabisa vilabu vya pombe kufunguliwa wakati wa kazi.

Muumini wa kanisa la Pentekoste (FPCT) Singida mjini, Metusela Daudi Kisuda,amempongeza rais Dk.John Pombe Magufuli kwa hatua yake makini na ya haraka, kuwajibisha watumishi wa umma wanao lewa pombe wakati wa kazi.

Muumini wa kanisa la Pentekoste (FPCT) Singida mjini, Metusela Daudi Kisuda,amempongeza rais Dk.John Pombe Magufuli kwa hatua yake makini na ya haraka, kuwajibisha watumishi wa umma wanao lewa pombe wakati wa kazi.

“Kwa ujumla pombe ni mbaya na ndio maana imesemwa pombe sio chai. Pombe inasababisha nguvu kazi nyingi ipotee. Nasisitiza tu kwamba kuanzia ngazi ya mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya hadi mwenyekiti wa Kijiji, wahakikishe nguvu kazi haipotei kwa kunywa pombe,” alisema Peter.

Alisema utamaduni wa kunywa pombe ukiachwa uendelee holela hata kipindi cha kazi, Taifa halitapona, litaangamia kwa vile litakuwa na watu legelege wenye afya mbovu.

Na Nathaniel Limu, Singida

Share:

Leave a reply