Rais Magufuli awaapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri wapya Ikulu Dar leo

498
0
Share:

Rais Dkt. Joseph Magufuli amewaapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri wapya na kisha ameweza kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri hao baada ya kumaliza kiapo chao Ikulu Jijini Dar es Salaam, kitendo kinachoashiria kuanza kazi mara moja kwa wateule hao.

Walichozungumza mawaziri wapya baada ya kuapishwa

Baada ya kuapishwa na Rais John Magufuli leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuanza kazi mara moja, Mawaziri na Manaibu Waziri wapya na waliobadilishiwa wizara, baadhi yao wamezungumzia mikakati yao ya utendaji kazi katika wizara zao.

Wakizungumza katika nyakati tofauti baada ya kuapishwa, Mawaziri hao wameahidi kushirikiana na timu ya mawaziri iliyokuwepo zamani kuwatumikia watanzania.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika  amesema atahakikisha anashirikiana na vyombo vya dola kutokomeza rushwa kwa watumishi wa umma pamoja na kuwadhibiti kutotoka katika ofisi zao wakati wa kazi kitendo kinachosababisha wananchi kukosa huduma kwa wakati.

“Nitaisimamia wizara vyema kwa kuhakikisha watumishi wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni na kufanya kazi katika maeneo yao ya kazi, wananchi wamekuwa wanakosa huduma sababu watumishi wamekwenda kunywa chai. Watumishi wa umma lazima walipwe mshahara kamili kwa kufanya kazi kamili, nitajitahidi kwa kushirikiana na Takukuru kutoa elimu kwa wananchi wa ajili ya kutokomeza rushwa,” amesema.

Aidha, Mkuchika ameahidi kuwepo uwazi kwa viongozi wa umma ili wananchi wajue kinachofanywa na serikali yao.

“Nitahakikisha mahusiano kazini yanaimarika baina ya mwajiri na mwajiriwa, ziko kanuni zinawezesha mwajiri na mwajiriwa kufanya kazi vizuri na vyombo vya usuluhishi vinafanya kazi, ili kila mmoja aheshimu mkataba wake wa kazi.”

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema atashirikiana na wizara ya Ardhi kuhakikisha anaondoa migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima.

“Migogoro ya ardhi, ni changamoto lakini ilani ya ccm ya uchaguzi imeelekeza migogoro hii kuisha kwa kuhakikisha inatengwa ardhi na kuwagawia wakulima na wafugaji, jambo hili ni la wizara nyingi, ikiwemo ya ardhi na kilimo, pia jambo hili lipo ofisi ya waziri mkuu linafanyiwa kazi ili wafugaji na wakulima wanufaike na watanzania wanufaike. Lazima tufanye kazi kwa ajili ya kujenga uchumi wa nchi,” amesema.

Kwa upande wake Waziri Mpya wa Wizara ya MaliAsili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla ameahidi kuja na mbinu mpya katika kuvutia utalii ili sekta hiyo iweze kukua zaidi, huku akituma salamu kwa watu wanaojishughulisha na vitendo vya ujangili kuacha mara moja kwani amejipanga kutokomeza ujangili nchini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amemshukuru Rais Magufuli kwa kumteua na kuahidi kufanya mabadiliko katika wizara yake, ikiwemo kuhakikisha habari zinapatikana kwa usahihi na kwa wakati, pia ameahidi kupandisha hadhi ya lugha ya Kiswahili ili izidi kutambulika ulimwenguni na kuwa chanzo cha ajira kwa watanzania.  

Mawaziri na Manaibu Mawaziri hao pamoja na Wizara zao ni pamoja na:

 1. Wizara ya Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora.

Waziri – George Huruma Mkuchik

2.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira

Waziri – January Makamba

Naibu Waziri – Kangi Lugola

3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu

Waziri – Jenista Mhagama

Naibu Waziri – Anthony Peter Mavunde

Naibu Waziri Walemavu – Stela Alex Likupa

4.Wizara ya Kilimo

Waziri – Charles John Tizeba

Naibu Waziri – Mary Mwanjelwa

5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Waziri – Makame Mbarawa

Naibu Waziri – Atashasta Nditiye

Naibu Wziri – Elias John Kwandikwa

6.Wizara ya Fedha na Mipango

Waziri – Dr Philip Mpango

Naibu Waziri – Dr Ashatu Kijaji

7. Wizara ya Nishati

Waziri – Medrad Matogoro Kalemani

Naibu Waziri – Subira Hamisi Mgalu

 1. Wizara ya Madini

Wairi – Angela Kairuki

Naibu Waziri – Haroon Nyongo 

9. Wizara ya Katiba na Sheria

Waziri – Palamagamba Kabudi

 1. Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Waziri – Agustino Mahiga

Naibu Waziri – Dkt Susan Kolimba

11 .Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Waziri – Dr Hussein Mwinyi

 1. Wizara ya Mambo ya Ndani

Waziri – Mwigulu Nchemba

Naibu Waziri – Hamad Masauni

 1. Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Waziri – William Lukuvi

Naibu Waziri – Angelina Mabula

 1. Wizara ya Maliasili na Utalii

Waziri – Hamisi Kigwangala

Naibu Waziri – Ngailonga Josephat

 1. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Waziri – Charles Mwijage

Naibu Waziri – Stella Manyanya

 1. Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi

Waziri – Joyce Ndalichako

Naibu Waziri – William Ole Nasha

17 .Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Waziri – Ummy Mwalimu

Naibu Waziri – Faustine Ndugulile

 1. Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo

Waziri – Dr . Harrison Mwakyembe

Naibu Waziri – Juliana Shonza

 1. Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Waziri – Isack Kamwelwe

Naibu Waziri – .Juma Hamidu Aweso

 1. Mifugo na Uvuvi

Waziri – Luhaga Mpina

Naibu Waziri – Abdallah Ulega

 1. Wizara ya TAMISEMI

Waziri – Suleiman Japho

 Na Regina Mkonde

 

Share:

Leave a reply