Rais Magufuli awataka wananchi wafanye kazi ili vyuma viachie

115
0
Share:

Rais Dkt. John Magufuli ameeleza namna ya kupunguza ukali wa ugumu wa maisha ambapo baadhi ya watu hufananisha hali hiyo na vyuma kubana, ambapo amesema ili kuvifungua vyuma vilivyobana inatakiwa watu wafanye kazi.

Magufuli ametoa mbinu hiyo mapema leo Machi 14, 2014 Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma wakati akihutubia katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa-Standard Gauge kutoka Morogoro hadi Dodoma. 

“Huu ndio wakati wa kuajiri watanzania, vya bure hakuna, asiye fanya kazi na asile na asipo kula afe hii ndiyo lugha ya ukweli na siku zote tutawaambia ukweli, kama kuna miradi hii yote watanzania wanatakiwa kufanya kazi. Halafu mtu analalalamika njaa, alalamike vyuma vimebana amejibanisha mwenyewe, vyuma avingue kwa kufanya kazi,” amesema.

Amesema serikali yake inajibu suala la upungufu wa ajira kwa vitendo  kwa kuanzisha miradi mikubwa ambayo inatoa ajira kwa watanzania wengi, na kusema kuwa mradi huo aliouzindua leo utatoa ajira zaidi ya 30,000  za moja kwa moja na 6,000 zisizo za moja kwa moja ukianza kutekelezwa.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply