Rais Magufuli, Mo Dewji watuma salamu siku ya wanawake

201
0
Share:

Tarehe 8 Machi ya kila mwaka dunia inaadhimisha Siku ya Wanawake, ambayo hutumika kutoa heshima kwa juhudi mbalimbali ambazo zinafanywa na wanawake katika nyanja mbalimbali.

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Mohammed Enterprises, Mohammed Dewji wameungana na watu wengine duniani kuwatakiwa wanawake maadhimisho mema kwa kutambua mchango wao katika maisha yao.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Magufuli ameandika, “Nawapongeza wanawake wote kwa kusherehekea siku yenu ya leo na hasa kwa mchango wenu mkubwa mnaoutoa kwa jamii. Daima tutaendelea kuwaheshimu, kuwapa ushirikiano na kutambua juhudi zenu katika kujenga ustawi wa jamii yetu.”

Nae Dewji ameandika, “Hakuna binadamu bila mwanamke! Lazima tuwashukuru kwa mchango wenu na tuendelee kuhimizana na kuwanyanyua wanawake wote. Kwa kweli mchango wao katika maisha yetu hauelezeki. Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awabariki wanawake wote.”

Share:

Leave a reply