Rais Magufuli,Rais benki ya Dunia watumia usafiri wa Mwendokasi kutoka Ikulu hadi Ubungo Dar

969
0
Share:

Machi 20.2017 majira ya saa tano kasoro, katika eneo la Ubungo Maji Watanzania walipata kumshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akiwasili kwenye eneo la tukio la uwekaji wa jiwe la msingi kwenye makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma ujenzi wa barabara za juu (Ubungo Interchange) Ubungo, jijini Dar es Salaamwa sambamba na ugeni wake akiwemo Rais wa Benki ya Dunia  (WB) Bwana  Jim Yong Kim ukiwasili hapo kwa kutumia mabasi ya Umma ambayo ni ya Mwendokasi (UDART).

MO Blog iliweza kushuhudia shangwe za wananchi baada ya Mshehereshaji kuwatangazia kuwa, Mh. Rais na ugeni wake wanawasili kwa kutumia Mabasi hayo, wananchi mbalimbali walilipuka kwa shangwe na kila mtu alikuwa na hamu ya kutoka kuona tukio hilo.

Hii ni  mara ya pili Rais Magufuli anatumia mabasi hayo ya Mwendokasi huku tukio linguine ni lile lililofanyika wakati ule wa uzinduzi rasmi wa mradi huo ambapo pia aliweza kuzindua kwa kupanda ndani ya mabasi hayo yeye na ujumbe wake wakiwemo wageni waalikwa, mawaziri na maafisa wa serikali.

Wananchi: MO blog iliweza kushuhudia umati mkubwa ndani ya eneo la shughuli hiyo sambamba  na nje ya barabara ambapo umati mkubwa ulikusanyika ukishuhudia tukio hilo la aina yake.

Awali katika vituo hivyo vya Mwendokasi, MO Blog iliweza kushuhudia ulinzi kuimalisha ndani ya vituo vya mwendokasi hasa hicho cha Ubungo Maji sambamba na maeneo yote ya jirani ya eneo la ufunguzi wa tukio hilo.

Hata hivyo baada ya uzinduzi huo kufanyika  wananchi  ambao walikuwa barabarani, waliweza kupaza sauti kutaka wasikie sauti yake pamoja na salamu, hali ambayo Rais aliweza kukubali na kuwasalimia wananchi hao na kuwapongeza huku akiwataka kuwa wa kwanza kulinda miundombinu yote ya miradi hiyo.

Basi la Mwendokasi lililokuwa limewabeba viongozi wakuu akiwemo Rais Magufuli na wageni wake wengine likiwasili  eneo la ubungo.

Basi hilo likiwasili eneo hilo la Ubungo Maji

Viongozi mbalimbali pamoja na Ugeni wa Rais wa Benki ya Dunia ukishuka katika basi hilo la Mwendokasi

Rais Magufuli akishuka katika basi hilo la Mwendokasi akiwa pamoja na mgeni wake, Rais wa Benki ya Dunia.

Rais Magufuli akiwatambulisha viongozi wa Serikali kwa mgeni wake Rais wa Benki ya Dunia (kushoto)

Rais Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika tukio hilo sambamba na Rais wa benki ya Dunia

Baadhi ya wananchi wakishuhudia kwa mbali tukio hilo

Rais Magufuli (kulia) akifuatiwa na Rais wa Benki ya Dunia, Waziri wa TAMISEMI Mh. Simbachawene na Waziri wa Fedha, Mh. Mpango wakiwa katika picha ya pamoja baada ya tukio hilo.

NB: PICHA ZOTE NI MALI YA MO BLOG, Tafadhari na Marufuku kupakua bila idhini ya wamiliki. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaopakua picha ama andishi la habari hii na kutumia katika mitandao yao ikiwemo Blogs.

Share:

Leave a reply