Rais mstaafu wa awamu ya Pili, Mh. Hassan Mwinyi atembelea banda la Zantel Sabasaba

571
0
Share:

Rais mstaafu wa awamu ya Pili, Mh. Hassan Mwinyi atembelea banda la Zantel katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere.

Katika ziata hiyo Mh. Mwinyi pia ameweza kupata maelezo mbalimbali jinsi mtandao huo unavyofanya kazi zake na utoaji huduma kwenye maonyesho hayo.  Miongoni mwa huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel ni pamoja na huduma za mawasiliano, huduma za intaneti.

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili wa Tanzania Mhe. Ally Hassan Mwinyi (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri (wa tatu kushoto) juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel jana jijini Dar es salaam baada ya kiongozi huyo kutembelea banda la Kampuni hiyo katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili wa Tanzania Mhe. Ally Hassan Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mfanyakazi wa Zantel Fadhili Mfinanga (wa pili kushoto) juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel jana jijini Dar es salaam baada ya kiongozi huyo kutembelea banda la Kampuni hiyo katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere.

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili wa Tanzania Mhe. Ally Hassan Mwinyi (wa pili kulia) akipokea mfuko wa zawadi baada ya kiongozi huyo kutembelea banda la Kampuni ya Mawasiliano Zantel ili kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Katikati ni Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri.

Mkazi wa Mbagala, Husna Hamisi akichangia damu katika banda la Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel alipotembelea banda hilo kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam. Zantel kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa damu Salama wameandaa utaratibu wa uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa huduma hiyo katika kipindi hiki cha maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Anayetoa damu kushoto ni Msanifu Maabara kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Sebastian Magulu. Kulia ni Meneja wa Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa.

Share:

Leave a reply