Rais Nkurunziza atangazwa kuwa kiongozi milele

214
0
Share:

Chama tawala nchini Burundi CNDD/FDD kimetangaza Rais wa nchi huyo, Pierre Nkurunziza kuwa ni kiongozi mkuu asiye na kikomo cha utawala ndani ya chama hicho.

Uuamuzi huo umefikiwa baada ya kufanyika vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa CNDD/FDD uliofanyika eneo la Buye lililoko Kaskazini mwa Burundi ambako Nkurunzinza alizaliwa. 

Uamuzi huo umechukuliwa wakati Burundi ikiwa inajiandaa kufanya marekebisho ya katiba li kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelea kuliongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.

Aidha, taarifa ya chama cha CNDD/FDD imeeleza kwamba, vikao hivyo pia vilikuwa na lengo la kuimarisha chama hicho na taasisi zake.

Share:

Leave a reply