Rais Obama amteua kwa mara ya kwanza Muislam kuwa Jaji Mkuu nchini Marekani

267
0
Share:

Rais wa Marekani Barack Obama ameweka historia nchini Marekani kwa kumteua Bwana Abid Quresh Mmarekani ambaye ni Muislam kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya wilaya ya Columbia nchini humo.

“Ninayofuraha kumchagua Bw. Qureshi kutumikia kwenye benchi la mahakama ya moja ya wilaya ya Marekani na nina uhakika kwamba atawatumikia wananchi wa amerika kwa uadilifu na kujitolea mbele ya haki” amesema Obama.

Bw,Qureshi ni mzaliwa wa Pakistani ambaye ni mshirika katika moja ya kituo cha sheria cha ’Latham and Watkins LLP’ lakini pia ni mwenyekiti katika kampuni maarufu duniani ya ‘Pro Bono’

Ijapokuwa Rais Obama anatarajiwa kuachia ofisi ya ikulu lakini uteuzi huo wa bw,Qureshi bado haujapitishwa na seneti ya nchini humo.

Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC)

Share:

Leave a reply