Rais Trump na Rais Putin uso kwa uso kwenye mkutano wa G20

623
0
Share:

Rais wa Marekani, Donald Trump wiki ijayo anataraji kukutana kwa mara ya kwanza na Rais wa Urusi, Vladimir Putin katika mkutano wa nchi 20 zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani (G20) ambao utafanyika nchini Ujerumani.

Taarifa ya viongozi hao wa mataifa makubwa duniani kukutana imetolewa na Mshauri wa usalama wa taifa Marekani, H.R. McMaster ambaye licha ya kuthibitisha Trump na Putin kukutana alisema bado haijajulikana watazungumza nini.

“Haijajulikana ni jambo gani watazungumza, inaonekana watazungumza mambo ambayo wataamua wao wenyewe,” alisema H.R. McMaster wakati akitoa taarifa kuhusu Rais Trump kuhudhuria mkutano wa G20.

 

Mkutano huo wa G20 unatarajiwa kufanyika Julai, 7 na 8 na viongozi wa mataifa mbalimbali ambao ni wanachama wa G20 watashiriki na mwenyeji wao akiwa ni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Share:

Leave a reply