Rais wa 42 wa Marekani atangaza kuacha kupokea misaada kutoka kwa wahisani

234
0
Share:

Aliyekuwa Rais wa 42 wa Marekani Bill Clinton amesema Taasisi yake ya ‘Clinton Foundation’ itaacha kupokea misaada na michango kutoka mashirika mbalimbali endapo mkewe Bi Hillary Clinton atashinda katika uchaguzi wa Novemba mwaka huu.

Clinton ametangaza pia kuacha kutoa hotuba za kulipwa ambazo amekua akizifanya kati ya sasa na siku ya uchaguzi, lakini pia atajitoa katika bodi ya wakurugenzi ya taasisi hiyo kama mkewe Bi.Hillary Clinton atashinda uchaguzi nchini Marekani.

Uamuzi huo wa Clinton utazuia lakini si kuondoa tofauti na migongano ya kimaslahi katika taasisi hiyo ya ‘Clinton Foundation’ ambayo kwa sasa inaongozwa na Rais huyo mstaafu pamoja na mkewe ambaye anatarajiwa kushiriki katika uchaguzi hapo mwezi Novemba.

Moja kati ya sheria za uchaguzi nchini Marekani zinamzuia mgombea wa Urais kupokea misaada na pesa kutoka katika mashirika mbalimbali kama mgombea ,lakini sheria hiyo haizuii mashirika hayo au mtu yeyote kusaidia au kuchangia taasisi ama mfuko wowote unaomilikiwa na familia ya mgombea.

Aidha Taasisi ya ‘Clinton Foundation’ imefanya kazi kubwa  sana ulimwenguni kwa kukuza sekta za afya kimataifa na kupigania haki za binadamu ulimwenguni na wafadhili wake wamesaidia ukuaji wa taasisi hiyo kwa ujumla.

Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC)

Share:

Leave a reply