Rais wa Jamhuri ya Congo leo kufanya mazungumzo na Donald Trump kuhusu Afrika

965
0
Share:

Rais wa Jamhuri ya Congo, Denis Sassou Nguesso leo jumanne ya Desemba, 27 anataraji kukutaa na kufanya mazungumzo na Rais mteule wa Marekani, Donald Trump kuhusu machafuko yaliyojitokeza Libya na mambo mengine ambayo yanahusu bara la Afrika kwa ujumla.

Taarifa ya Sassou na Trump kukukutana imetolewa na msemaji wa Sassou, Thierry Moungalla kupitia akaunti yake ya Twitter ambapo aliandika kuwa pamoja na kukutana watafanya mazungumzo jinsi gani wanaweza kusaidia kumaliza kabisa machafuko ya Libya na kutatua changamoto ambazo zinalikabili bara la Afrika.

Aidha kwa upande wa Donald Trump hawajatoa taarifa yoyote kuhusu kukutana kwa Sassou na Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ambaye anataraji kuingia madarakani mwezi Januari 20, 2017 akichukua nafasi ya Barack Obama.

Share:

Leave a reply