Rais wa Msumbiji awatimua mawaziri wanne

500
0
Share:

Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi amewafukuza kazi mawaziri wanne, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Nishati.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Rais Nyusi, inaeleza kwamba hakuna sababu zilizotajwa ambazo zimechangia kufukuzwa kazi mawaziri hao, pia taarifa hiyo haikutaja mawaziri walioteuliwa kujaza nafasi hizo.

 Mawaziri waliofukuzwa ni, Leticia da Silva Klemens ambaye alikuwa Waziri wa Nishati, Oldemiro Baloi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara na wa Kilimo na Usalama wa Chakula.

Share:

Leave a reply