rais wa sos children’s village aahidi kuimarisha ushirikiano na Tanzania utoaji wa huduma kwa watoto

220
0
Share:

Rais wa SOS Children’s Village, Siddhartha Kaul amesema taasisi hiyo itaendelea kuimarisha ushirikiano na serikali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuendelea kusaidia miradi mbalimbali inayohusu kuwalinda watoto hapa nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Ijumaa katika ziara yake ya siku nne nchini Tanzania, alisisitiza kwamba kupitia SOS Children Village ataendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania ili kuangazia masuala mbalimbali yanayoathiri usalama wa watoto nchini Tanzania.

“Tutaendelea kufanya kazi na jamii pamoja na serikali katika kuweka mazingira mazuri ya baadaye kwa watoto ili kuhakikisha huko mbeleni wanatimiziwa mahitaji yao muhimu,” alisema.

Ziara ya Rais huyo ilianzia Zanzibar ambako alitumia fursa hiyo kutembelea watoto na kukagua baadhi ya miradi ambayo inatekelezwa na asasi hiyo.

Kwa Dar es Salaam Kaul atakutana na watoto na kukagua miradi michache ambayo inasimamiwa na asasi hiyo pamoja na kubadilishana mawazo na viongozi mbalimbali wa Serikalini.

Kuhusu SOS Tanzania Bara na Zanzibar

SOS Children’s Villages Tanzania na Zanzibar ni asasi huru isiyo ya serikali na taasisi ya maendeleo ya jamii iliyosajiliwa Tanzania na Zanzibar inayohusiana na SOS Children’s Village International yenye makao makuu yake Innsbruck, Austria.

SOS Children’s Villages imelenga kufanya kazi za watoto ambao wamekosa malezi na wale ambao wapo kwenye hatari ya kukosa matunzo.

SOS inatoa malazi bora kwa kila mtoto. Tunawapa watoto hawa fursa kujenga uhusiano wa kudumu ndani ya familia na kuwasaidia kutengeneza maisha yao ya baadaye. Kwa sasa SOS CV TZ inafanya kazi zake Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Iringa (Iringa Mjini na Mufindi), Zanzibar (unguja na Pemba)

Rais wa SOS Children’s Village, Siddhartha Kaul (kulia) akiwasili katika kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS Children’s village kilichopo Ubungo jana jijini Dar es salaam. Rais huyo yupo nchini kwa ziara ya siku 2 ambapo atakagua miradi ya shirika hilo na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa SOS Village Tanzania, Dk. Mary Nagu.

 

Meya wa Ubungo, Boniface Jocob akisalimiana na mmoja wa wasimamizi wa  kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS Children’s village kilichopo Ubungo jana jijini Dar es salaam. wakati wa tukio hilo la Rais huyo ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku 2 ambapo atakagua miradi ya shirika hilo na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa SOS Village Tanzania, Dk. Mary Nagu.

Kikundi cha watoto wanaolelewa katika makazi ya SOS children’s village Ubungo jijini Dar es salaam, kikitoa burudani ya aina yake wakati wa hafla ya kumpokea rais wa Shirika hilo ambaye aliwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku 4 mwishoni mwa juma. Raisi wa Shirika hilo ameweza kukagua miradi ya SOS Children’s village na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali.

Rais wa SOS Children’s Village Siddhartha Kaul, akisalimiana na watoto wanaolelewa katika kituo cha SOS Children’s village kilichopo Ubungo hivi karibuni jijini Dar es salaam. Rais wa Shirika hilo alitua nchini kwa ziara ya siku 2 ambapo alikagua miradi ya shirika hilo na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali.

Rais wa SOS Children’s Village Siddhartha Kaul, na Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob wakikagua baadhi ya nyumba zinazotumiwa na watoto wanaolelewa katika kituo cha SOS Children’s village kilichopo Ubungo hivi karibuni jijini Dar es salaam. Rais huyo alitua nchini kwa ziara ya siku 2 ambapo alikagua miradi ya shirika hilo na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali.

Rais wa SOS Children’s Village Siddhartha Kaul, akizungumza wakati wa hafla ya kukaribishwa nchini Tanzania mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Rais huyo alitua nchini kwa ziara ya siku 2 ambapo alikagua miradi ya shirika hilo na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali.

Share:

Leave a reply