RASMI Lazaro Nyalandu ajiunga Chadema

761
0
Share:

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amejiunga rasmi na chama cha CHADEMA leo katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani jijini Mwanza.

Baada ya kukabidhiwa kadi ya Chadema, Nyalandu ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram,“NASIMAMA mbele yenu na mbele ya Watanzania wote nikiwa nimeisubiri kwa shauku kubwa siku hii ya leo ili nipate fursa ya KUJIUNGA na harakati za kupiganiq mageuzi ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi nchini Tanzania, kwa kujiunga Rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema. Asanteni sana kwa upendo wenu na mapokezi makubwa! 

Nilijiondoa CCM Oktoba 30 mwaka huu na kujiuzulu nafasi yangu ya Ubunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya CCM, ikiwa ni pamoja na kujivua nafasi zote za Uongozi ndani ya CCM, ikiwepo Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, kwa kuwa katika miaka miwili ya Uongozi wa Awamu ya Tano, nimeamini na kujiridhisha kuwa CCM imepoteza mwelekeo, na kwamba niliporejea “Ahadi za Mwanachama wa CCM”, nikakumbushwa maneno haya:

Nitasema KWELI daima, na UONGO kwangu mwiko. Katika Majira na nyakati tunazozipitia kama Taifa, 
Na mimi “Naogopa kusema UONGO”. Mabadiliko ya kisiasa ni lazima nchini Tanzania, na Wakati ni huu.

Wakati wa kuondoka CCM, nililijulisha Taifa azma yangu ya kutaka kujiunga na Chadema, endapo Wana Chadema wataona VEMA, kuniruhusu niingie malangoni mwenu. Niwe mmoja wenu, tushikamane pamoja!

Wakati naondoka CCM, nililijulisha TAIFA kuwa, daima nitakuwa mwaminifu kwa nchi yangu Tanzania, na kwamba naungana na Upinzani kupigania HAKI, kwa kuwa imeandikwa HAKI huinua TAIFA, na kwa pamoja tutaitafuta na kuilinda tunu hii muhimu kwa TAIFA letu.

Wakati naondoka CCM, nililijulisha TAIFA kuwa naamini kwamba, Tanzania inahitaji kupata Katiba Mpya, na kwamba tufanye rejea ya RASIMU ya mapendekezo ya Katiba ya Tume ya Warioba ili pamoja na Mambo mengine, kuwepo mgawanyo kamili wa madaraka katika mihilimi ya utawala wa Chini (Bunge, Serikali, na Mahakama), na kuondoa muingiliano na kuweka ukomo wa madaraka wa wazi kwa kila muhimili.”

Mwanza, Tanzania Mh. Freeman Mbowe, Mb. Mwenyekiti wa Chadema-Taifa Mh. Dr. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema-Taifa Mh. Ezekiel Wenje, Mwenyekiti wa Kanda ya Mwanza Mh. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema: Mh. Godbless Lema, Wah. Viongozi wa Kanda, Mh. Mgombea Udiwani Kata hii Ndugu Wana Chadema, Ndugu Wananchi Wote mliohudhuria, Ndugu Wanahabari, Mabibi na Mabwana: AMANI IWE NANYI: PEOPLES! POWER! NASIMAMA mbele yenu na mbele ya Watanzania wote nikiwa nimeisubiri kwa shauku kubwa siku hii ya leo ili nipate fursa ya KUJIUNGA na harakati za kupiganiq mageuzi ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi nchini Tanzania, kwa kujiunga Rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema. Asanteni sana kwa upendo wenu na mapokezi makubwa! Nilijiondoa CCM Oktoba 30 mwaka huu na kujiuzulu nafasi yangu ya Ubunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya CCM, ikiwa ni pamoja na kujivua nafasi zote za Uongozi ndani ya CCM, ikiwepo Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, kwa kuwa katika miaka miwili ya Uongozi wa Awamu ya Tano, nimeamini na kujiridhisha kuwa CCM imepoteza mwelekeo, na kwamba niliporejea “Ahadi za Mwanachama wa CCM”, nikakumbushwa maneno haya: Nitasema KWELI daima, na UONGO kwangu mwiko. Katika Majira na nyakati tunazozipitia kama Taifa, Na mimi “Naogopa kusema UONGO”. Mabadiliko ya kisiasa ni lazima nchini Tanzania, na Wakati ni huu. Wakati wa kuondoka CCM, nililijulisha Taifa azma yangu ya kutaka kujiunga na Chadema, endapo Wana Chadema wataona VEMA, kuniruhusu niingie malangoni mwenu. Niwe mmoja wenu, tushikamane pamoja! Wakati naondoka CCM, nililijulisha TAIFA kuwa, daima nitakuwa mwaminifu kwa nchi yangu Tanzania, na kwamba naungana na Upinzani kupigania HAKI, kwa kuwa imeandikwa HAKI huinua TAIFA, na kwa pamoja tutaitafuta na kuilinda tunu hii muhimu kwa TAIFA letu. Wakati naondoka CCM, nililijulisha TAIFA kuwa naamini kwamba, Tanzania inahitaji kupata Katiba Mpya, na kwamba tufanye rejea ya RASIMU ya mapendekezo ya Katiba ya Tume ya Warioba ili pamoja na Mambo mengine, kuwepo mgawanyo kamili wa madaraka katika mihilimi ya utawala wa Chini (Bunge, Serikali, na Mahakama), na kuondoa muingiliano na kuweka ukomo wa madaraka wa wazi kwa kila muhimili,

A post shared by LazaroNyalandu (@lazaronyalandu) on

Share:

Leave a reply