Ray C bado yupo yupo, asema ataendelea kutoa nyimbo

340
0
Share:

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Rehema Chalamila, maarufu kama Ray C ameweka wazi juu ya mwenendo wake wa muziki wake kwa kusema bado ataendelea kutoa nyimbo siku hadi siku kadri muda unavyokwenda

Ray C ambaye pia ameshirikishwa katika nyimbo ya Chege iliyotoka hivi karibuni ya ‘najiuliza’ amesema kwa sasa watu wategemee kazi zaidi baada ya kuwa kimya muda mrefu

“Nyimbo zipo nyingi kwa hiyo watu wategemee kuziskia tu, mashabiki wangu wasubiri kusikiliza tu,” alisema Ray C.

kwa muda mrefu sasa Mwanadada huyo tangu alipokuwa kimya katika muziki kwa shutuma za utumiaji wa madawa ya kulevya ambapo inasemekana lilikuwa tatizo sugu kwake kuacha, ingawaje hakusema kilichomuweka kimya kwenye muziki kwa muda wote huo

“Nafikiri kilichotokea dunia nzima inajua siwezi kusema,” aliongeza Ray C.

Mwanadada Ray c,sasa ameamua kuja kwa nguvu zote kwenye muziki huku akisema ameandaa nyimbo nyingi ambazo ziko tayari kilichobaki ni kuziachia kwa muda sahihi,lakini miongoni mwa hizo nyimbo hakuna msanii kutoka nje ya Tanzania.

Na Rahimu Fadhili

Share:

Leave a reply