RC Gambo akutana familia na watoto walionusurika ajali ya basi la Lucky Vicent

487
0
Share:

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo  leo Agosti 22,2017  amekutana na familia za wazazi wa watoto  watatu ambao watoto wao walinusurika na ajali ya gari iliyotokea Mei sita mwaka huu na kusababisha vifo vya wanafunzi 32 na walimu 2 na dereva 1 wa shule ya Lucky Vicent ya mkoani Arusha.

Watoto hao ni pamoja na  Dorene Mshana, Wilson Tarimo na Sadia Ismail  ambao tayari wapo nchini  baada ya kurejea kutoka  Marekani walikokwenda kwa ajili ya matibabu  kutokana na ajali hiyo,  leo Agosti 22,2017 wameweza kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo amewajulia hali pamoja na kupata kuzungumza nao mambo mbalimbali pamoja na wazazi wa watoto hao.

Katika tukio hilo, Mkuu wa Mkoa Mh. GAmbo aliweza kuwakabidhi  kila mmoja kiasi cha Tsh. 7,750,000 kila familia ili ziwasaidie kwenye masuala yao mbalimbali ikiwemo Elimu.

“Nimeona utukufu wa Mungu kupitia watoto hawa!,” alieleza RC Gambo wakati wa tukio hilo.

Mkuu wa Mkoa Mh. Gambo akikabidhi kiasi cha Tsh. 7,750,000 kila familia ili ziwasaidie kwenye masuala yao mbalimbali ikiwemo Elimu.

Mkuu wa Mkoa Mh. Gambo akisalimiana na mmoja wa watoto hao 

Mkuu wa Mkoa Mh. Gambo akisalimiana na mmoja wa watoto hao 

Mkuu wa Mkoa Mh. Gambo akikabidhi kiasi cha Tsh. 7,750,000 kila familia ili ziwasaidie kwenye masuala yao mbalimbali ikiwemo Elimu.

Mkuu wa Mkoa Mh. Gambo akiwa katika picha ya pamoja na watoto hao

Mkuu wa Mkoa Mh. Gambo akiwa katika picha ya pamoja na watoto hao

Share:

Leave a reply