RC Singida ampa Mkurugenzi siku 14 kujenga banda la wafanyabiashara wa vitunguu Misuna

398
0
Share:
Soko la Vitunguu Misuna

Mkuu wa mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe amefanya ziara ya kushutukiza katika soko la wakulia na wafanyabiashara wa vitunguu wa soko la kimataifa  Misuna ambapo alimpa siku 14 Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Singida, Deus Lisige awe amejenga kibanda kwa ajili ya wauza vitunguu hao, waweze kujihifadhi wakati wa mvua na jua.

Mathew Mtigumwe

Mkuu wa mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe (kulia mwenye miwani) akimwagiza Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Singida, Deus Lisige (anayeaangalia kamera), kwamba ahakikishe ndani ya siku 14 awe amejenga kibanda kwa ajili ya wakulima na wafanyabishara wa vitunguu soko la kimataifa Misuna, waweze kujihifadhi wakati wa mvua na jua.

Joseph Nandoo

Mwenyekiti wa SACCOS ya wafanyabiashara wa vitunguu soko la kimataifa la Misuna mjini Singida, Joseph Nandoo (mwenye fulana ya misitari), akimweleza jambo Mkuu wa mkoa wa Singida, mhandisi Mathew Mtigumwe (mwenye suti nyeusi), aliyetembelea soko hilo.

Mathew Mtigumwe

Mkuu wa mkoa wa Singida,mhandisi Mathew Mtigumwe, akikagua soko la vitunguu la kimataifa la Misuna mjini Singida alipofanya ziara ya ghafla ya kikazi na kuagiza manispaa kujenga soko la kisasa la vitunguu,ili kuvutia wakulima ndani na nje ya mkoa,kuuzia vitunguu vyao.

IMG_4490

Baadhi ya wakulima, wafanyabiashara na vibarua katika soko la vitunguu la kimataifa la Misuna, wakiendelea na majukumu yao wakati mkuu wa mkoa wa Singida,mhandisi Mathew Mtigumwe alipolitembelea soko hilo.(Picha zote na Nathaniel Limu)

Share:

Leave a reply