ROMA Mkatoliki aelezea jinsi walivyotekwa

1555
0
Share:

Baada ya mkasa uliompata Msanii wa Muziki wa Hip Hop nchini, Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’ pamoja na wenzake watatu hivi karibuni, amesema kwa sasa hawezi kufikiria kuendelea kufanya shughuli za muziki hadi pale hali yake kiafya itakapotengemaa.
Akisimulia mkasa mzima mbele ya Waziri mwenye dhamana ya Sanaa, Dkt. Harisson Mwakyembe, Roma amesema bado usalama wao ni mdogo na kuvitaka vyombo vya dola kuwaongezea ulinzi.

“Kwa sasa tuangalie afya yangu, mziki ni hisia huwezi kushika peni na karatasi na kuanza kuandika mistari na pia akili yangu jinsi ilivyo ni ngumu kuandika. Hivyo muziki siyo kitu ninachoweza kufikiria kwa sasa,” amesema na kuongeza.

“Hatuna uhakika wa usalama wetu tulipokuwepo si pazuri, kama hili tukio alifanyiwa daktari, msanii na mwanasiasa usishituke ukisikia limemkuta mwandishi wa habari, tulipotoka eneo hilo kila mmoja alimshukuru Mungu. Tunaomba vyombo vituongezee ulinzi vituonezee usalama Waziri lifikishe kwenye vyombo husika, na wale wa kwenye majukwaa wapaze sauti zao kukemea halii sababu nina hofu tutaendelea na tabia hii,”

Roma amewashangaa baadhi ya wasanii waliomtuhumu kujiteka ili kutafuta kiki kwa kuandikwa kwenye vyombo vya habari.

“Habari za kusikitisha watu wanasema tunfanya kiki ili tuandikwe kwenye vyombo vya habari kwa masilahi ya kisanii, wengine wanasema tumepewa hela na wanasiasa kuichafua serikali, vitu hivi vinatusumbua sana. Tunatafuta ridhiki kupitia muziki sisi ni watu masikini,” amesema.

Share:

Leave a reply