Roma Mkatoliki afungiwa miezi sita, Nay Wa Mitego apewa onyo

447
0
Share:

Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imemfungia msanii wa muziki wa kizazi kipya Roma Mkatoliki kutofanya kazi yoyote ya sanaa ikiwemo maonyesho ya sanaa ya majukwaa kwa kipindi cha miezi sita na kumtaka Msanii Nay Wa Mitego kuacha kutumia maneno yenye utata yanayolenga kuleta mmomonyoko wa maadili.

Akizungumza wakati akitoa adhabu hiyo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alisema, “Naiagiza BASATA kuanzia sasa inapotokea kuna wimbo umetolewa na msanii yeyote na unakiuka maadili ya Mtanzania wimbo huo uchukuliwe hatua kwa haraka ili kuhakikisha kwamba sanaa kama msingi muhimu wa kuburudisha na kuelimisha inazingatia miiko na maadili yetu.”

Nae Katibu Mkuu wa Basata, Godfrey Mngereza aliwataka wasanii kufata maadili ya Kitanzania kwa kutunga nyimo ambazo pamoja na kuburudisha lakini pia ziwe zinatoa mafunzo kwa jamii.

“Wasanii fuateni misingi imara ya kuelimisha na kuburudisha kuliko kuleta athari katika jamii hasa kwa kizazi cha leo na cha kesho kwani BASATA haina budi kutumia kanuni na sheria zilizopo kuwajibisha kazi za sanaa ambazo zinaathiri jamii ya kitanzania kimaadili,” alisema Mngereza.

Share:

Leave a reply