Ronaldo ashinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ureno 2016

878
0
Share:

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno na mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ureno kwa mwaka 2016.

Akizungumzia ushindi huo, Ronaldo ameshukuru kwa ushindi huo na kusema, “Ulikuwa mwaka mzuri sana kwa kwangu kwa sababu nimeshinda Euro,

“Nawashukuru Wareno wote, walitufanya tujiamini na kutufanya tushinde kombe la Ulaya.”

Wengine walioshinda tuzo ni pamoja na kiungo wa Bayern Munich, Renato Sanches ambaye ameshinda Tuzo ya Mchezaji Chipukizi wa mwaka na kocha wa timu ya taifa ya Ureno, Fernando Santos akishinda Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka.

Share:

Leave a reply