Rooney awajibu wanaosema ameshuka kiwango

201
0
Share:

Tangu kuanza kwa msimu wa 2016/2017 wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wadau mbalimbali wa soka duniani wamekuwa wakimzungumzia nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney kuwa ameshuka kiwango.

Baada ya maneno kuwa mengi ambayo yanazungumzia kiwango chake, Rooney amezungumzia jambo hilo na kueleza kuwa yeye anafanya kitu ambacho anaagizwa kufanya na sio kuwasikiliza watu wengine.

“Namsikiliza kocha wangu na wachezaji wenzangu, watu ambao wapo karibu yangu na sisikilizi mambo ambayo watu wengi wanasema sababu mengi wanayozungumzia ni maneno machafu,

“Ninatakiwa kuwa makini, kujituma, na kweli nimeshalifanya hilo katika maisha yangu ya soka. Ninajituma sana na kujitahidi kuonyesha uwezo wangu kwa timu,” alisema Rooney.

Aidha Rooney amezungumzia matokeo ambayo timu yake imekuwa ikiyapata kwa siku za karibuni na kusema kuwa hicho ni kipindi cha mpito na anaamini watarejea katika kiwango bora.

“Tumekuwa na wiki mbaya, siku nane mbaya ambazo tulipoteza michezo mitatu, ni muhimu sasa kujipanga vizuri kwa ajili ya hilo na kuja na njia mbadala,” alisema Rooney.

Share:

Leave a reply