RPC Arusha awapa onyo wamiliki wa mabasi

284
0
Share:

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limetoa onyo kwa wamiliki wa mabasi ambayo yanavunja sheria za usalama barabarani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya matokeo ya ukaguzi wa mabasi ya abiria uliofanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 22 mwezi huu hadi 24, Kamamda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba, wamiliki wa magari wanatakiwa wahakikishe mabasi yao yanazingatia ubora unaokubalika hali ambayo itasaidia abiria wanasafiri salama. 

“Mbali na ubora wa gari lakini pia madereva wanatakiwa wazingatie sheria za usalama barabarani kama vile kuendesha kwa kufuata maelekezo ya alama,” alisema Kamanda Mkumbo. 

Alisema katika ukaguzi huo wa kushtukiza uliojumuisha mabasiyaliyokuwa yanakwenda mikoani na yale yaliyokuwa yanaingia jijini hapa, jumlaya mabasi 77 yalikamatwa kwa makosa yaubovu na mwendokasi. 

“Kati ya hayo mabasi 25 yalikamatwa kwa makosa ya mwendokasi ambapo 20 kati yao yalilipiwa tozo na matano wahusika walipelekwa mahakamani, wakati mabasi 52 yalikutwa na makosa ya ubovu ambapo 41 yalitozwa tozo na mabasi 11 toka makampuni mbalimbali tumeyasitishia kutoa huduma mpaka hapo yatakapofanyiwamarekebisho,” alifafanua Kamanda Mkumbo. 

Kamanda Mkumbo alisema kwamba pamoja na ukaguzi wa magarihayo ambao unafanywa kila siku lakini Jeshi hilo litaendelea kufanya kaguzi zakushtukiza mara kwa mara ili kuhakikisha abiria wa mabasi hayo wanasafirisalama, huku akitoa wito kwa abiria watoe taarifa popote wanapogundua derevaanakwenda kinyume na sheria za usalama barabarani.

Na Rashid Nchimbi – Jeshi la Polisi Arusha

Share:

Leave a reply